Jumatano, 28 Mei 2014

UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI

 Kuku: Jogoo na tembe
Kuku: Jogoo na tembe
Ulishaji: Kuku wa kienyeji wanaweza kulishwa kwa kumia mahindi, mchele, na mabaki ya ugali. Vyakula hivi ni lazima vikaushwe vizuri na kusagwa vizuri. Ulishaji ni lazima ufanyike katika sehemu safi au kwa kutumia vyombo vilivyotengenezwa maalumu kwa ajilii ya kulishia kuku.


Banda: Kuku wawe wa kienyeji au wa kisasa, wanahitaji kuwa na banda zuri kwa ajili ya malazi na kuwalinda. Wanahitaji chumba chenye nafasi ya kutosha na kinachopitisha hewa ya kutosha. Ni lazima kuwawekea fito kwa kuwa ndege hupenda kupumzika juu ya fito. Ni lazima banda la kuku lifungwe vizuri nyakati za usiku ili kuzuia wanyama wanaoweza kuwadhuru kuku. Ni lazima liwe safi wakati wote ili kuzuia magonjwa kama vile mdondo na mengineyo. Usitumie pumba za mbao au nguo kuukuu kwenye viota vya kutagia kwani huchochea kuwepo utitiri na funza wa kuku. Inashauriwa kutumia mchanga laini.


Maji ya kunywa: Kuku wapatiwe maji safi. Ni lazima kuangalia mara kwa mara na kuyabadilisha maji. Kamwe usiwape kuku maji machafu.


Chanjo: Chanjo kwa mifugo ni lazima ili kuzuia mashambulizi ya magonjwa. Magonjwa yaliyozoeleka ni kama vile Mdondo, Kideri, Ndui ya kuku, na homa ya matumbo (typhoid). Chanjo kwa kawaida hutolewa mara moja kwa kila baada ya miezi miwili.


Uwekaji wa kumbukumbu: Kumbukumbu zijumuishe aina ya ulishaji, namba ya uzalishaji, muda wa mwisho wa matumizi, kiasi cha malisho kwa kila siku, idadi ya vifo, na idadi ya mayai yaliyozalishwa.


Mwanzoni unahitaji nini?


Wafugaji walio wengi wanauliza wanahitaji nini katika hatua za awali ili kuweza kuanzisha mradi wa ufugaji wa kuku. Hii itategemea aina ya kuku uliochagua kufuga.


Ni busara kuwa na vifaa muhimu vinavyohitajika na viwe katika hali ya usafi kabla ya kuweka kuku bandani mwako. Kama unaanza na vifaranga, vifuatavyo ni vifaa muhimu vinavyohitajika kwa ajili ya vifaranga 200.


• Tenga na utengeneze banda zuri lenye joto na hewa ya kutosha wakati wote.
• Vyombo vinne (4) vya kunyweshea maji, hii ni katika wiki 2 za mwanzo na uongeze vyombo taratibu kulingana na kuku wanavyokua.
• Vyombo vinne (4) vya kulishia chakula, na viongezeke kulingana na kuku wanavyokua.
• Matandazo makavu na safi, inaweza kuwa maranda au mabua ya ngano.
• Pakiti moja au mbili za dawa ya Coccid (hii inapatikana katika maduka yote ya kilimo). Hata hivyo, utaratibu wa chanjo ni lazima ukamilishwe.
• Chakula kwa ajili ya vifaranga ambacho kimezalishwa na watengenezaji wanaoaminika.
chanzo:mkulima mbunifu

UJASIRIA MALI: UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI


DONDOO ZA UFUGAJI BORA KUKU WA ASILI

 
Muhtasari wa ufugaji kuku wa asili ili kuzuia vifo na kuboresha uzalishaji.
 
 
Ufugaji wa kuku wa asili ni nyenzo muhimu katika kupambana na wimbi la umasikini kwa kuongeza kipato cha kaya. Hata hivyo, pamoja na soko la uhakika, bado ufugaji kuku haujaweza kutumika ipasavyo kupambana na umaskini unaowakabili watanzania wengi. Ni mazoea kwa jamii nyingi hapa Tanzania kufuga kuku wa asili kama sehemu ya mila na desturi zao. Kuku wa asili amekuwa akifugwa bila ya kupatiwa huduma muhimu kama makaazi bora, chakula cha ziada, tiba, kinga za magonjwa mbali mbali . muhtasari huu unatoa muongozo wa ufugaji wa kuku wa asili ili uweze kuzalisha  na hatimae kukuza kuku kwa wingi.
 
 
Dondoo ya 1. Usafi wa vyombo na mazingira ya kuku
·         Uchafu ni mama wa magonjwa, hivyo zingatia haya;
·         Vyombo vya chakula na maji visafishwe mara kwa mara kwa maji na sabuni.
·         Pumba au chakula kilicholowana na kuchanganyika na kinyesi cha kuku vitolowe na kuzikwa.
·         Choma moto au zika kwenye shimo refu kuku waliokufa kwa ugonjwa.
·         Usifuge kuku na ndege wa jamii nyingine kwa mfano bata katika banda moja.
·         Ondoa mbolea mara kwa mara kutoka katika banda la kuku.
·         Tumia dawa za kuulia vimelea kusafishia banda na upake chokaa angalau mara moja kwa mwaka.
·         Ziba matundu yote yanayoweza kuruhusu panya na wanyama wakali kama vicheche kuingia katika banda la kuku.
 
 
Dondoo ya 2. Magonjwa na kinga kwa kuku wote.
 
 
Ndui ya kuku.
Huathiri sana vifaranga wanaokua na kujitokeza kwa wingi wakati wa mvua ndefu. Husababisha vivimbe katika uso/ kishungi na hata sehemu nyengine zisizo na mnyoa.
 
 
Mdondo/kideri
Mdondo, au kwa majina mengine lufuo, au kideri ni ugonjwa hatari kuliko kati ya magonjwa ya kuku wa asili. Ni ugojwa wa virusi ambao huathiri kuku wa rika zote, huweza kuangamiza kuku wote kijijni.
 
 
Ukosefu wa vitamin A
Ugonjwa huu husababisha macho kuvimba na kutoa uchafu mziito kama sabuni iliyolowana. Kuku wenye dalili hizi hawaponi na hata kufa. Ugonjwa hujitokeza baada ya kipindi kirefu cha kiangazi kwa ajili ya ukosefu wa majani mbichi.
 
 
Koksidiosisi
Huathiri kuku wa umri wowote lakini huuwa zaidi vifaranga na kuku wanaokuwa. Kuku hudhoofika manyoya huvurugika na kuku huwa kama wamevaa koti. Kuku huarisha damu au kinyesi cha kahawia na huzubaa na kuonekana kama wamevaa koti.
 
 
Viroboto, chawa na utitiri
Hawa ni wadudu wa n je wanaoshambulia ngozi. Huweza kusababisha ugonjwa kutokana na kunyonya damu. Viroboto hushambulia kichwa na kunata huku wakinyonya damu. Viroboto huuwa vifaranga. Chawa na utitiri hughasi kuku hadi wakashinwa kutaga na kuatamia.
 
 
Minyoo.
Minyoo huweza kudhofisha kuku na kuwafanya waweze kuugua maradhi mengine kirahisi. Muune mtaalaam ukihisis kuku wako wana minyoo.
 
 
Dondoo ya 3. Chakula cha ziada:
·         Wapatie vifaranga nyongeza ya protini kwa kuwachanganyia vumbi la dagaa au vichwa l vya dagaa vilivyotwangwa kwenye pumba za mahindi.
·         Changanya kikombe kimoja cha vumbi la dagaa na vikombe vitano vya pumba za mahindi (tumia kikombe kidogo cha chai) .
·         Mchwa na wadudu wengine wanaweza kutumika kam nyongeza ya protini.
·         Vuna mchwa kwenye vichuguu au tengeneza mchwa katika njia za mchwa.
·         Kutengeneza mchwa: changanya kinyesi cha ng’ombe na majani makavu, mabua ya mahindi au maranda ya mbao katika chungu au ndoo ya zamani.
·         Mwagia maji hadi kila kilichomo kirowane kisha weka katika chombo kama ndoo au chunngu. Weka chombo chako katika njia ya mchwa ukikigeuza juu chini na subiri hadi kesho yake asubuh, kisha beba vyote vilivyomo na uwamwagie kuku mahali walipo.
 
 
Dondoo ya 4. Utotoleshaji wa vifaranga;
 
 
Chagua jogoo bora na tetea bora kuzalisha kuku .
·         Sifa za jogoo bora ;
1.       Awe na umbo kubwa, awe ukiko mzuri na usioangukia upande mmoja.
2.       Apende kuwa na himaya yake. Ukimpata jogoo mwenye sifa hizi muweke yeye na matetea kumi. Hivyo ukiwa na matetea ishirini jogoo wawili wanatosha.
·         Sifa za tetea bora;
Tetea bora ni Yule mwenye umbo kubwa, mwenye uwezo wa kutaga mayai ya kutosha, kuatamia na hatimae kutotoa vifaranga na
·         Uhifadhi wa mayai;
1.       Weka mayai mahali safi na penye hewa ya kutosha.
2.       Tumia box lililokatwa na kujaza mchanga mkavu na safi au kasha la kuhifadhia mayai.
3.       Weka sehemu butu ya yai iwe upande wa juu na ile iliyochongoka itizame chini.
4.       Andika namba au tarehe katika siku lilipotagwa.
5.       Mayai yakishatagwa yatolewe na kuhifadhiwa na moja liachwe kwenye kiota ili kumuita kuku kuja kutaga kesho yake.
·         Kuatamiza mayai;
-          Kuku awekewe mayai yatakayokuwa na uwezo wa kuyaatamia na kuyatotoa yote.
-          Mayi 10 hadi 12 yanatosha kutamia.
-          Mayai ya kutamiza yasizid wilki 2 toka kutaga.
-          Yai la mwisho kutagwa liwe la kwanza kuchaguliwa hadi yapatikane mayai 10 mpaka 12, na apewe kuku kuyaatamia.
-          Mayi ya kutamiza yasafishwe kwa kitambaa kikavu  na safi au kilichowekwa spiriti
·         Kutotolesha vifaranga wengi kwa wakati mmoja.
-          Kama unataka kuku zaidi ya mmoja watamie na kutotoa kwa mpigo fanya yafuatayo;
-          Kuku wa kwanza akianza kuatamia muwekee mayai yasiyo na mbegu mfano mayai ya kuku wa kisasa au kuku asiye na jogoo.
-          Rudia zoezi hilo hadi utakapofikisha kuku watano kasha waweke kuku wote mayai yenye mbegu.
 
 
Dondoo ya 5. Matumizi ya vifaranga  ili kuzuia vifo.
Vifaranga wengi hufa kabla ya kufikisha miezi miwili kutokana na magonjwa, baridi na kuliwa na wanyama wengine. Ili kupunguza vifo vya vifarang wa siku 1 hadi miezi miwili zingatia yafuatayo;
Ulinzi dhidi ya mwewe na wanyama wengine.
Weka vifarang kwenye tega na kuwafunika ili wasinde mbali wakati wa mchana. Wape maji na chakula. Hakikisha hawapigwi jua wala kunyeshewa mvua. Wakati wa usiku walale na mama yao.
 
 
Chanjo ya mdondo kideri/lufuo
Kama tetea alichanjwa kabla ya kuanzakutaga vifaranga wanaoambuliwa huwa na kinga ya dondo ya kuwatosha kwa wiki 3 za kwanza za maisha yao. Wachanje vifaranga hao dhidi ya mdondo wafikishapo umri wa siku 18.
Vifaranga ambao historia ya chanjo ya mama haijulikani, wapewe chanjo ya mdondo siku tatu baada ya kuanguliwa, rudia wakifikisha wiki tatu kasha uchanje kila baada ya miezi 3  
Kinga dhidi ya kiksidiosisi
Kinga ya koksidiosisi kwa vifaranga, itolewe hata kama ugonjwa haujajitokeza.
·         Wape dawa ya aprolium kwa muda wa siku tatu mfululizo mara wafikishapo siku saba tokea waanguliwe kama kinga ya koksidiosisi.
·         Dawa inaweza kutolewa hata kama wamevuka umri huo. Fuata maelekezo ya mtaalam juu ya kiasi cha dawa kinachopaswa kuchanganwa  katika maji au pumba
·         Kama vifaranga wadoga wataonesha dalili za kuzubaa kama kuvua koti wapewe dawa ya amprolium kwenye maji kwa utaratibu ufuatao;
Dawa siku tatu mfululizo: usiwape kwa siku mbili; gawa tena kwa siku tatu
 
 
HITIMISHO
Hakikisha banda na vyombo vya chakula cha kuku na visafi kuepusha magonjwa.
·         Usichanganye kuku na bata katika banda moja
·         Lisha chakula cha ziada hasa kwa vifaranga.
·         Kideri, koksidiosisi, ndui na upungufu wa vitamin  A ni vyanzo vikuu vya vifo vya kuku wako. Kumbuka kukinga kuku wako dhidi ya magojwa haya.
·         Kumbuka kuchagua mayai ya kuatamiza kama ilivyoelekezwa ili kuepuka kupata mayai viza.
·         Vifaranga wadogo hadi wiki nane huhitaji matunzo mazuri fuata maelezo kuzuia vifo.
·         Kumbuka ukiuza kuku wengi kwa mpigo utaongeza mapato yako, jitahidi kuzalisha vifaranga kwa wingi ili upate kuku wengi baadae.
·         Muone mtaalam wa mifugo ulie karibu nae kwa ushauri zaidi.
·         Soma maelezo haya mara kwa mara na ufanye yalioelekezwa.
·         Washirikishe wengine katika kaya yako ili nao wajifunze na kufanya, ivyo kukuza ufugaji na kipato cha familia.

UFUGAJI BORA WA KUKU WA KIENYEJI


UJASIRIAMALI---UFUGAJI BORA WA KUKU WA WKIENYEJI

Idadi ya wanyama wanaofugwa kwa chakula imezidi ile ya binadamu zaidi ya mara mbili kote ulimwenguni. Kuna maelfu ya wanyama kote duniani ilihali ni wachache tu wanaoweza kufugwa. Kati ya hawa wanyama, ni aina nne (Ng'ombe, kondoo, mbuzi na kuku) wanaochukua asilimia 95% ya wanyama wote wanaofugwa. Wanyama hawa hupatikana katika nchi za hari kwenye nyanda za chini. Lakini kati ya mifugo hawa, kuku ni maarufu katika nchi za hari na hata kote ulimwenguni.Lengo la makala hayayai kutoa maelezo ili kusaidia wafugaji wa kiwango kidogo katika nchi
zinazostawi, katika kupunguza umaskini. Sehehe ya kwanza (I) itatoa maelezo kuhusu ufugaji na
hasa ufugaji wa kuku, Sehemu ya pili (II) itaangazia maswala yafuatayo katika kuinua hali ya uchumi
kwa kufuga kuku: 
1. Kuendeleza ufugaji wa kuku za kienyeji kwa kutumia n na zisizohitaji gharama nyingi.
2. Kutafuta mbinu na a ia muafaka za kuzalisha viwango vya kuku bora kwa njia ya kiasili.
3. Matumizi ya njia za kiasili au zile zisizo gharimu pesa nyingi kutibu na kuzuia magonjwa ya
kuku.
SEHEMU YA I: MAELEZO KUHUSU UFUGAJI WA KUKU KATIKA NCHI
ZINAZOENDELEA
 
NAFASI YA MIFUGO
Licha ya kukosa mashamba makubwa ya kuendeleza ufugaji wa ng'ombe, jamii nyingi katika nchi za hari (tropics) hupata nafasi ya kufuga kuku kwa kiwango kidogo. Idadi ya wanyama wanaofugwa huongezeka sambamba na ile ya watu. Idadi ya watu inapoongezeka ndipo ile ya mifugo huzidi.
Idadi kubwa ya watu huhitaji chakula kingi na matumizi huongezeka, hivyo basi watu hufanya bidii kuzalisha chakula na mapato kutoka kwa shamba.
Ufugaji wa ng'ombe na wanyama wanaohitaji lishe kwa wingi huhitaji kiasi kikubwa cha shamba ili kupanda mimea na lishe la mifugo. Ukilinganisha na ufugaji wa kuku, utahitaji mabaki ya vyakula na sehemu ndogo ya shamba. Ufugaji wa kuku umeweza kunawiri hata pasipo fedha.
Katika nchi za hari ufugaji wa kienyeji hautahititi kazi nyiyii, kazi hii hufanywa na akina mama na watoto. Kwa kawaida katika nchi hizi kazi nyingi za nyumbani h hekelezwa na mama. Vyakula vya kuku vyaweza kutoka kwa: 1) Mabaki ya chakula, 2) Mabaki ya mimea, 3) Mabaki kutoka jikoni na 4) Vyakula vya kujitafutia (kwa mfano kwekek, mbegu, wadudu, nyongonyongo, n.k). Mfumo wa kufuga kuku kwa njia ya kienyeji hutumia viungo vinavyopatikana kwa urahisi na kuimarisha hali ya kiuchumi na chakula bora kwa jamii.
Ni muhimu sana kufuga mifugo hata ikiwa ni kwa kiwango kidogo kwa sababu ya 1) Chakula bora na kuongeza mapato ya jamii kwa viwango vya kuridhisha; 2) Mifugo ni hakiba au banki, faida yake huzaana tu kama riba ya benki; 3) Mifugo yaweza kuuzwa ili kugharamia karo ya wanafunzi, malipo ya hospitali, gharama nyingine za nyumbani na hata shambani; 4) Kwa matumizi ya kijamii (kwa mfano kulipia mahari, shughuli za kidini, n.k); 5) Mifugo husaidia katika kukabili wadudu, kwekwe na kuimarisha rutuba k kokana na mbolea ya kinyesi. Ni bayana kwamba m mugo ni muhimu sana kwa mkulima yeyote yule.
UMUHIMU WA UFUGAJI WA NJIA YA KIENYEJI
Ufugaji wa kuku katika nchi zinazostawi waweza kugawanywa mara mbili: 1) Ufugaji wa
kitamaduni au kienyeji pasipo kuwepo gharama, na 2) Ufugaji wa kisasa unaohitaji fedha nyingi.
Ufugaji wa viwango vikubwa kwa kuzingatia mfumo wa kisasa ni maaruru katika kuzalisha kuku wa nyama na wale wa mayai. Mfumo huu hujumuisha asilimia ndogo sana ya aina ya ufugaji.
Itafahamika kwamba mfumo wa kisasa haujaadhiri ule wa kienyeji. Idadi kubwa ya watu katika nchi za hari hutegemea mfumo wa kienyeji kwa nyama na mayai.
Mfumo wa kisasa huhitaji pesa nyingi za kununua vyakula vya kuku. Aidha mfumo wa kisasa huhitaji kazi nyingi ili kutekeleza. Mfumo wa kisasa umefaulu katika nchi zilizostawi kutokana na hali nzuri ya kiuchumi katika kuzalisha (kuku wa hali
ya juu, kuangua vifaranga kwa stima, vyakula vilivyo na madini mengi, vifaa na zana za mashine, utaalamu wa hali ya juu n.k). Haitafaa sana kuanzisha mfumo kama huu katika vijiji vya mataifa yanayostawi.
"Mageuzi" katika ufugaji (kuambatanisha mfumo wa kisasa pamoja na ule wa kienyeji) yamefanyiwa majaribio katika mataifa yanayostawi tangu miaka ya 1950. Matokeo ya kuku wapatao 200 hadi 300 kwa shamba moja hayajawai kufaulu. Hasara imepatikana na waweza kuona nyumba zilizokuwa na kuku bila chochote, pesa nyingi zimepotea na kuku hawapo.
Mfumo wa kienyeji ni bora (Katika hali ya kiuchumi) iwapo idadi ya kuku haitazidi kuku 50. Ni rahisi kuweza kuwatunza kuku, kwani hakuna gharama nyingi. Iwapo vyakula au zana za kisasa zitanunuliwa, basi haitakuwa k k viwango vikubwa. Mazao ya nyama na mayai yataleta faida.
Sehemu nyingi katika mataifa yanayostawi hakuna stima, katika nchi za hari, ufugaji kwa kiwango > dogo umeweza kufaulu na kuimarisha uchumi.
 
FAIDA ZA UFUGAJI WA KUKU KWA NJIA YA KIENYEJI
Faida za uzalishaji kuku ili kuimarisha uchumi kwa njia hii zimepuuzwa na viongozi na wafadhili.
Kuku huleta faida kwa jamii kama tulivyoona katika sehemu ya I. Zaidi ya hayo, ufugaji wa kuku waweza kuimarishwa pasipo gharama nyingi ukilinganisha na mifugo wengine.
· Hutupatia fedha kwa kuuza nyama na mayai
· Mayai ni chakula kilicho na madini muhimu na kisicho ghali katika soko lolote. (madini kama methionine na cystine), madini haya ni muhimu sana kwa afya ya watu hasa watoto wachanga. Pia hutupatia protini.
· Kinyesi cha kuku ni mbolea safi
· Kiwanda asilia cha kutotoa vifaranga
· Gharama za kuanzisha na kuendeleza ni nyepesi
· Kitoweo chepesi na rahisi kwa wageni, kitoweo hakihitaji hifadhi hutumika mlo mmoja au miwili na kumalizika
· Jogoo hutumika kama saa inapowika
· Manyoya ya kuku hutumika kutengenezwa mapambo mbalimbali, mito na magodoro
· Kuku wanahisimu wadudu waharibifu
Kuku ndiye mnyama wa kipekee anayeweza kuishi mahali popote hapa ulimwenguni bila kuadhiriwa
na viwango vya hali ya hewa. Ufugaji wa kuku ndio shughuli inayofanyika kwa wingi duniani kuliko ufugaji wa aina yeyote. Kuku hunawiri vyema katika nchi za hari kutokana na uwiano uliopatikana wakati wa mwanzo binadamu alipofuga Asian jungle fowl aina ya kuku-mwitu. Mayai pia yaweza kuhifadhiwa kwa urahisi na huchukua nafasi ndogo kuliko aina ya bidhaa zozote za mifugo. Mayai yaweza kuwekwa mahali kwa muda mrefu bila kuhitaji barafu. Hautahitaji kuhifadhi kuku kwa njia yoyote, kwani nyama yake hupatikana pale unapohitaji kwa kuchinja.
Upungufu wa kuku wa kigeni ukilinganisha na wale wa kienyeji ni kama ufuatao:
• Kuku wa kigeni hawawezi kukalia na kuangua mayai, hivyo basi wahitajika kununua vifaranga (gharama);
• Vifaranga wa kigeni huhitaji utunzaji maalum na vyakula maalum (gharama);
• Kuku waliozalishwa kwa njia ya kisasa huhitaji chakula kingi ili kututa mayai (g(grama);
• Kuku wa kisasa huhitaji zaidi kuchanjwa dhidi ya magonjwa (gharama)ukilinganisha na w wkienyeji (japo nao huhitaji chanjo);
• Kuku wawautaga mayai huhitaji mwangaza wa stima (saa 14 kwa siku) ili kutaga mayai (gharama)
Kwa kuongezea, rangi ya nyama na mayai ya kuku wa kienyeji huvutia kuliko ile ya kuku wa kisasa.
Hivyo basi jaribu kuendeleza na kuhimiza ufugaji wa kuku za kienyeji.
Iwapo mkulima ana jogoo mmoja na kuku kumi na mbili, basi kila mwezi waweza kupata kuku akikalia mayai 10-12 kwa mwezi (mayai yote kwa wakati mwingi hayataanguliwa) kuna hakikisho la kupata vifaranga vinne kila mwezi. Kuku mzima atachukua miezi minne kuchunga vifaranga walioanguliwa. Kwa hivyo, kati ya kuku wote kumi na mbili kila mara kutakuwa na kuku wanne wakitunza vifaranga, huku wale wengine wanane wakitaga mayai.
Kuku waliofugwa kwa njia ya kitamaduni hupata vyakula vyao kwa kutafuta mbegu, wadudu nyongonyongo, n.k; Lakini kuku hawa hukosa vyakula vya kutosha vilivyo na nguvu ili waweze kutaga mayai. Vyakula vya kutoa nguvu daima huwa ni haba.
Waweza kuwalisha kuku kwa nafaka ili wapate chakula cha nguvu (mfano kilo moja ya nafaka iliyopondwa kila siku kwa kuku 10), nafaka hii yapaswa kuwa kavu. Vifaranga wapewe kiasi kidogo cha nafaka au mchele wiki za kwanza. Kuku wanaolishwa nafaka baada ya kujitafutia chakula nje huongeza idadi ya mayai (kutoka asilimia 20-25% hadi 40-50%). Kuna umuhimu wa kuhifadhi nafaka kama lishe badala ya kuuza kwani utapata mayai mengi ambayo baadaye utaweza kuuza.
Hautahitaji kununua vyakula vya protini kwani kuku hujitafutia lishe la protini.
Ikiwa hauna nafaka, waweza kutumia vyakula vya mzizi au ndizi. Vyakula vya aina hii hata hivyo, huwatatiza kuku wanapovitonogoa, kiwango cha mayai sio kikubwa kama cha wale wanaolishwa nafaka.
Kwa kuwalisha kuku kwa nafaka utapata hakikisho la mayai manne kwa siku kutoka kwa wale kuku wanane. Iwapo hakuna nafaka, kati ya kuku wanane wanaotaga utapata mayai mawili tu kwa siku.
Ni bora kutumia nafaka hii kama lishe kuliko kuuza na hatimaye kununua vyakula vya dukani.
Kuku kumi na mbili na jogoo mmoja wanaolishwa kwa kilo moja ya nafaka kila siku waweza kuelezwa hivi:
• Waweza kuuza kuku wanne kila mwezi na kujaza pengo hilo na wale vifaranga (vifaranga wanne huanguliwa kila mwezi) na
• Dazani kumi za mayai kila mwezi (mayai manne kila siku).
Kwa mwaka mmoja waweza kukadiri ile faida utakayopata na vile hali ya kiuchumi yaweza kuinuliwa katika mataifa yanayostawi.
Hata hivyo faida hii haitaafikiwa iwapo magonjwa hayatazuiwa au kukabiliwa kama ifuatavyo.
TEKELEZA UTARATIBU WA KUZUIA MAGONJWA
Magonjwa ndio husababisha hasara katika mfumo wa ufugaji wa kuku. Kuku waliochanjwa dhidi ya magonjwa hudumisha afya bora. Jaribu kila mara kuzuia magonjwa, kwani kuzuia ni bora kuliko kuponya. Kinga yaweza kutolewa mara kwa mara (kila baada ya miezi mitatu) dhidi ya magonjwa
yafuatayo:
Ugonjwa wa Newcastle
Ugonjwa huu ndio huadhiri kuku na kusababisha hasara katika nchi za hari. Virusi vya ugonjwa huu huenea kwa kasi na rahisi kiasi cha kusababisha vifo kwa asilimia 100%. Dalili za kwanza ni shida ya kupumua na kung'amua hewa, sauti kama ya kikohozi na kutokwa mate. Kinyesi chaweza kuwa na rangi ya kijani kibichi. Hadi sasa hakuna dawa.
Waweza kuzuia ugonjwa huu kwa kutoa chanjo. Dawa za chanjo hupatikana kote ulimwenguni hata katika nchi za hari kwenye vipimo vya vitone mia moja. Madawa haya yaweza kuhifadhiwa kwa muda. Waweza kuweka kwa wiki moja mbali na jua au joto kali (Chanjo hii ni ya kipekee, kwani aina nyingine ya chanjo huwekwa kwa friji). Waweza kutoa chanjo kwa kutia vitone kwenye mdomo. Kuku wote (wakubwa kwa wadogo) wapaswa kupewa chanjo baada ya kila miezi mitatu.
Minyoo
Minyoo kama chango (roundworms) na tegu (tapeworms) huadhiri kuku wa kienyeji. Kuku hukosa hamu ya chakula, mayai hupungua na magonjwa mengine hushambulia. Ni bora basi kutoa minyoo.
Mchanganyiko wa madawa ya aina tatu ndio hutumiwa kuangamiza minyoo, madawa haya ni piperazine, phenothiazine na butynorate. Madawa haya hupatikana kama vidonge (tumia kidonge 1 kwa kuku mzima na 1/2 kwa vifaranga). Iwapo hautapata dawa hii, waweza kutumia Panacur au dawa nyingine ya kuangamiza minyoo. Wapatie kuku dawa ya minyoo kila baada ya miezi mitatu.
Wadudu
Wadudu kama chawa au utitiri husumbua kuku katika ufugaji wa kienyeji. Chawa au utitiri husababisha harara ya ngozi, kuku walio adhiriwa hupata shida na kukosa usingizi. Hali hii hupunguza kiwango cha mayai na uzito wa kuku.
Tumia asilimia 5% ya unga wa malathion kwa kupulizia kuku (puliza kwa chupa uliyo toboa mashimo) pulizia kila kuku ili kuzuia chawa na utitiri (kilo moja ya unga huu yaweza kutibu kuku 150). Pulizia dawa hii baada ya kila miezi mitatu, waweza kupuliza kwa wakati mmoja wa kutoa chanjo na dawa zilizotajwa hapo juu. Puliza unga huu pia kwenye viota vya kuangulia mayai.
Waweza kutayarisha 5% ya malathion kwa kuchanganya 25% ya unga wa malathion (kiwango cha kilimo) na sehemu nne za jivu kutoka jikoni.
Magonjwa ya mapafu
Magonjwa ya mapafu huadhiri njia inayopitisha hewa na kuambatanisha mate na sauti kama ya kikohozi. Ugonjwa huu huenea polepole. Uambukizanaji pia hutokea kwa polepole na vifo sio kwa wingi. Hata hivyo, kutaga mayai na uzito hupungua. Shida hii yaweza kusambaa hata kutoka mahali vifaranga huanguliwa hadi pale walipouzwa.
Tylosin19 ndio dawa inayoweza kutibu magonjwa ya mapafu. Kiasi cha 35mg ya tylosin hutosha kuku mmoja (kiwango hiki hufaa kuku na hata vifaranga) dawa hii husimamisha madhara kutokana na magonjwa ya mapafu. Tibu kuku kila baada ya miezi mitatu, waweza kutekeleza kwa wakati mmoja wa kutoa kinga na kuangamiza minyoo. Tylosin hupatikana kwa pakiti ndogo ya 4gm.
Waweza kutayarisha dawa hii kwa kutumia maji na 35gm ya tylosin (gramu nne kwa vikombe viwili vya maji), kiasi hiki chaweza kutolewa kwa vitone kwa kila kuku.
.............................. ....//.............................. .
KWA UFUPI (SUMMARY)
Kabila za Kuku
Si rahisi kupata kabila halisi (pure breed) au kizazi halisi (pure line) zazauku wa kienyeji kutokana na mwingiliano wa vizazi kati ya aina mbalimbali za kuku hao. Lakini hata hivyo baadhi ya kuku wa kienyeji wanaweza kutambuliwa kutokana na maumbile yao kwa mfano
1. Kuchi



  • Warefuna wenye kusimama mgongo ukiwa wima
  • Wananaanyoya machache mwilini na vilemba vyao ni vidogo
  • Mayai gram 45

2. Ching'wekwe (Umbo dogo)


  • Hupatikana zaidi Morogoro na umasaini
  • Majogoo kilo 1.6
  • Mitetea kilo 1.2
  • Yai gram 37
  • kuku hawa wanafaa sana kwa biashara ya mayai kwa kuwa hutaga mayai mengi sana.

3. Umbo la Kati


  • Majogoo kilo 1.9
  • Mitetea kilo 1.1
  • Mayai gramu 43
  • Hukua upesi na hupata kinga upesi baada ya kuwachanja dhidi ya ugonjwa wa Mdondo (New Castle)

4. Singamagazi


  • Hupatikana zaidi Tabora
  • Majogoo wana rangi ya moto na mitetea rangi ya nyuki
  • Majogoo kilo 2.9
  • Mitetea kilo 2
  • Mayai gramu 56

5. Mbeya


  • Wanapatikana Ileje Mbeya na asili yao ni Malawi
  • Mjogoo kilo 3
  • Mitetea kilo 2
  • Mayai gramu 49
  • Uwezo wao wa kuatamia mayai na kuangua ni mdogo sana ukilinganisha na kuku wengine

6. Pemba


  • Maumbo ya wastani na miili myembamba
  • majogoo kilo 1.5
  • mitetea kilo 1
  • mayai gramu 42

7. Unguja


  • Hawatofautiani sana na wa Pemba
  • Vilemba vyake ni mchanganyiko- vidogo an vikubwa
  • Majogoo kilo 1.6
  • Mitetea kilo 1.2
  • Mayai gramu 42

SIFA WA KUKU WA KIENYEJI


  1. Wastahimilivu wa Magonjwa
  2. Wana uwezo wa kujitafutia chakula
  3. Huatamia, kutotoa na kulea vifaranga
  4. Wanastahimili mazingira magumu(ukame, baridi n.k)
  5. Nyama yake ina ladha nzuri

KATIKA KUWAENDELEZA KUKU WA KIENYEJI NI VYEMA


  1. Wajengewe nyumba bora
  2. Wapewe kinga dhidi ya ugonjwa wa Mdondo (New Castle), Ndui (Fowl Pox) pamoja na kinga ya minyoo.
  3. Malezi bora ya vifaranga
  4. Kuwapatia chakula cha ziada pamoja na maji ya kunywa ya kutosha.

NYUMBA BORA
Eneo inapojengwa nyumba au banda la kuku liwe


  • Linafikika kwa urahisi
  • Limeinuka juu pasituame maji
  • Pasiwe na pepo zinazovuma

Vifaa kama miti, nyasi, makuti, fito, udongo mabanzi ya miti, cement, mabati n.k
Sifa za Nyumba Bora ya Kuku


  • Paa imara lisilovuja
  • Kuta zisiwe na nyufa
  • Sakafu isiwe na nyufa
  • Madirisha ya kutosha kupitisha hewa
  • Iwe na mlango wa kuingia kufanya usafi
  • Iwe na ukubwa (nafasi) unaolingana na idadi ya kuku. Wastani wa kuku 10-15 kwa mita moja mraba

Mambo muhimu ndani ya nyumba


  • Chaga za kulalia kuku
  • Sakafu iwekwe maranda (wood shavings), makapi ya mpunga, n.k
  • Viota vya kutagia mayai sentimita 35x35x35 na idadi ya viota iwe nusu ya idadi ya kuku waliofikia hatua ya kutaga na viwekwe sehemu iliyojificha (faragha)

UATAMIAJI WA MAYAI
Kuna njia 2


  • Njia ya kubuni (incubators)
  • Asili

Kumuandaa kuku anayeatamia


  • Weka maranda au majani makavu ndani ya kiota
  • Anapokaribia kuatamia toa mayai ndani ya kiota pamoja na maranda, hakikisha mikono haina manukato
  • Nyunyiza dawa ya kuua wadudu (viroboto, utitiri n.k) ndani ya kiota, pia mnyunyizie dawa kuku anayetarajia kulalia mayai
  • Rudisha mayai kwenye kiota ili kuku aanze kuatamia
  • Kwa kawaida kuku hulalia mayai yake kwa muda wa siku 21 ndipo huanguliwa

ULEAJI WA VIFARANGA
Kuna njia mbili


  • Njia ya kubuni
  • Njia ya asili

Njia ya ASILI
Kuku mwenyewe hutembea na vifaranga akivisaidia kutafuta chakula. Ni vizuri kumtenga kuku mwenye vifaranga katika chumba chake pekee ili vifaranga wasishambuliwe na kuku wengine hali kadhalika kuwalinda na wanyama na ndege wanaoshambulia vifaranga.
Njia ya KUBUNI
Vifaranga huwekwa kwa pamoja kwenye chumba maalum na kupatiwa joto maalum, chakula pamoja na maji. Tumia taa ya kandili (chemli), umeme au jiko la mkaa na hiyo taa iweke kwenye mzingo(mduara) walipo vifaranga. Pia kuna kifaa kinaitwa Kinondoni Brooder ni kizuri kwa kutunzia vifaranga. Kwa kutumia kifaa hiki kuku wanaweza kunyang'anywa vifaranga vyao mara tu baada ya kutotoa na kuviweka kwenye hii brooder na hao kuku wakaachwa bila vifaranga vyao, baada ya majuma matatu au manne, kuku hao huanza tena utagaji na kuendelea na uatamiaji hadi kutotoa tena. Kwa mtindo huu kuku anaweza kutotoa mara 5-6 badala ya kama ilivyo sasa mara 2-3 kwa mwaka. Vifaranga vikae ndani ya brooder majuma 3-4 na baadaye fungua milango ya brooder kuruhusu vifaranga vitoke na kuzungukazunguka chumbani bila kuvitoa nje kw kipindi cha mwezi mmoja au zaidi kutegemeana na mazingira.
KULISHA KUKU WA KIENYEJI
Kuku mkubwa huhitaji gramu 120 za chakula kwa siku, ni vizuri kuku wanaofugwa huria (free range) kupatiwa chakula cha ziada gramu 30 kila siku nyakati za jioni.
Kuku walishwe


  • Mizizi-mihogo, viazi vitamu, mbatata, magimbi, n.k
  • Nafaka-mahindi, Mpunga, Mtama, Ulezi na Pumba za nafaka zote
  • Mboga-Mikundekunde, nyanya, milonge, majani ya mapapai
  • Matunda-Mapapai, maembe, n.k
  • Mbegu za Mafuta-Karanga, ufuta, mashudu ya pamba, alizeti, n.k
  • Unga wa dagaa
  • Maji

KUCHANGANYA CHAKULA CHA KUKU


  • Pumba.............kilo20
  • Mashudu ya Pamba n.k...kilo 3
  • Dagaa iliyosagwa.........kilo 1
  • Unga wa majani uliokaushwa kivulini na kusagwa........kilo 2
  • Unga wa Mifupa ..........kilo 0.25
  • Chokaa ya mifugo ........kilo 0.25
  • Chumvi........................ gramu 30
  • Vichanganyio/Premix...gramu 25

KUPANDISHA


  • Uwiano wa mitetea na jogoo ni mitetea 10-12 kwa jogoo mmoja
  • Sifa za mtetea ni mkubwa kiumbo, mtagaji mayai mengi, muatamiaji mzuri na mlezi wa vifaranga
  • Sifa za jogoo ni awe mkubwa kiumbo, miguru imara na yenye nguvu, mrefu, upanga/kilemba kikubwa, awe na uwezo wa kuitia chakula mitetea na awe na tabia ya kupenda vifaranga
  • Jogoo huanza kupanda akiwa na umri wa miezi 7-10 na kuendelea hadi miaka mitatu na asipande watoto wake
  • Mitetea huanza kutaga wakiwa na miezi 6-8

MAGONJWA YA KUKU
1. Mdondo/New castle
Virus vinavyosababisha ugonjwa huu huenezwa kwa hewa
Dalili


  • Kuhalisha choo cha kijani na njano
  • Kukohoa na kupumua kwa shida
  • Kupinda shingo kwa nyuma
  • Kuficha kichwa katikati ya miguu
  • Kukosa hamu ya kula na kunywa
  • Idadi kubwa ya vifo hadi 90%

Kinga


  • Chanjo (New Castle vaccine) kwa mpango wa siku 3, wiki 3, miezi 3
  • Epuka kuingiza kuku wageni
  • Choma au fukie mizoga ya kuku waliokufa kwa ugonjwa
  • Zingatia usafi wa mazingira

NDUIYA KUKU/ FOWL POX
Virus huambukizwa kupitia jeraha au mbu
Dalili


  • Vidonda vyenye utando wa kahawia/purple kwenye sehemu zinazoonekana
  • Kukosa hamu ya kula
  • Vifo vingi

Kinga


  • Chanja vifaranga wanapofikia mwezi 1-2 kwa kutumia chanjo ya Fowl pox vaccine
  • Epuka kuingiza kuku wageni
  • Zingatia usafi wa mazingira

HOMA YA MATUMBO/FOWL TYPHOID


  • Kuharisha kinyesi cha kijani na nyeupe
  • Kuku hukosa hamu ya kula
  • Kuku hukonda
  • Vifo hutokea kidogo kidogo kwa muda mrefu
  • Kinyeshi hushikamana na manyoya

Tiba
Dawa aina ya antibiotic, sulfa na vitamini
Kinga


  • Usafi
  • Fukia mizoga
  • Usiingize kuku wageni
  • Chinja kuku wote mara ugonjwa huu ukiingia na safisha banda, pia pumzika kufuga kwa miezi 6

MAFUA YA KUKU/INFECTIOUS CORYZA
Hutokana na bakitelia na hushambulia hasa kuku wakubwa
Dalili


  • Kuvimba uso
  • Kamasizilizochanganyikana na usaha unaonuka
  • Macho huvimba na kutoa machozi na pengine upofu
  • Hukosa hamu ya kula
  • Mbawa huchafuka na kutoa harufu mbaya

Tiba
Dawa za Antibiotic, sulfa na vitamini
KUHALISHA DAMU/COCCIDIOSIS
Husababishwa na vijidudu vya Protozoa
Dalili


  • Kuharisha damu
  • Manyoya husimama
  • Hulala na kukosa hamu ya kula

MINYOO
Dalili


  • Kunya minyoo
  • Hukosa hamu ya kula
  • Hukonda au kudumaa
  • Wakati mwingine hukohoa

Tiba
Dawa ya minyoo/Pipeazine citrate kila baada ya miezi mitatu
WADUDU
Viroboto, chawa, utitiri
Dalili


  • Kujikuna na kujikung'uta
  • Manyoya kuwa hafifu
  • Rangi ya upanga kuwa hafifu
  • Ngozi kuwa nene, ngumu na yenye magamba yanayodondoka kama unga

Kuzuia


  • Ziba mipasuko sakafuni na kwenye kuta za banda
  • Fagia banda mara mbili kwa wiki
  • Nyunyiza majivu au chokaa mara moja kwa wiki mara baada ya kufagia
  • Choma masalia ya mayai yaliyoanguliwa
  • Nyunyiza dawa kwenye viota
  • Weka maranda, majani makavu, makapi ya mpunga ya kutosha sakafuni ndani ya banda la kuku
  • Fuata kanuni za chanjo
  • Tenga kuku wagonjwa wakae mbali na kuku wazima

UPUNGUFU WA VIINI LISHE KWENYE CHAKULA
Dalili


  • Kuku hupungua damu, uzito na kudumaa
  • Mifupa huwa laini na kutokuwa imara
  • Hutaga mayai yenye gamba laini na madogo
  • Huwa na manyoya dhaifu,
  • source:http://www.jamiiforums.com/ujasiriamali/196005-kwa-wale-wanaotaka-kufuga-kuku-wa-kienyeji-kwa-ujasiriamali.htmlhttps://www.facebook.com/fredy.seka.9?ref=tn_tnmnhttps://www.facebook.com/fredy.seka.9?ref=tn_tnmn

Jumanne, 27 Mei 2014

Ufugaji kuku wa kienyeji na faida zake

TANZANIA inakadiriwa kuwa na idadi ya kuku wa kienyeji wanaofugwa milioni 34.
Idadi hii ya kuku bado ni ndogo ikilinganishwa na mahitaji halisi ya Watanzania.
Ufugaji wa kuku ni nyenzo nzuri ya kujipatia kipato katika kaya kwa sababu ufugaji huo hauhitaji mtaji mkubwa na hauna kazi kubwa kiuendeshaji.
Katika ufugaji huria kuku hujitafutia chakula wenyewe, pia inapowezekana hupewa mabaki ya chakula, chenga,
pumba au nafaka yoyote inayopatikana katika mazingira husika.
Kwa walio wengi ifikapo nyakati za jioni, kuku hulala jikoni au ndani nyumbani kwa mfugaji mwenyewe.
Ufugaji huu ni rahisi kwa kuwa hauna gharama kubwa ila faida yake ni kitoweo tu au fedha kidogo sana.
Kutokana na lishe duni na kuzaana wenyewe kwa wenyewe (bila kubadili jogoo), kuku wa kienyeji walio wengi wana uzito mdogo.
Wana wastani wa uzito wa robo tatu za kilo hadi kilo moja wakiwa na umri wa zaidi ya mwaka mmoja.
Ila wakitunzwa vizuri zaidi na kuboreshwa wana uwezo wa kufikia uzito wa kilo moja hadi moja na nusu katika umri wa miezi sita hadi nane.
Kwa upande wa utagaji wa mayai kuku 100 wa kienyeji kwa wastani hutaga mayai 50 hadi 65 kwa siku. Wakitunzwa vizuri zaidi huweza kufikia uzalishaji wa mayai 80 hadi 100 kwa siku.
Takriban wiki tatu zilizopita vijana wa Dar es Salaam walipata fursa ya kuhudhuria semina ya Kamata Fursa Twenzetu iliyoandaliwa na Kampuni ya Clouds Media Group ambapo lengo kuu lilikuwa ni kuwahamasisha vijana wa Kitanzania kuchangamkia fursa zilizopo kwa ajili ya kujiongezea kipato na kuepuka kubweteka kwa kusubiri ajira kutoka serikalini na kwenye kampuni mbalimbali nchini.
Katika semina hiyo mwezeshaji aliyeonekana kuwa kivutio ni Yahaya Nawanda ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida ambaye alitoa mada ya faida ya kufuga kuku wa kienyeji.
Nawanda anasema alianza na kuku wawili ambao alipewa zawadi na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo kabla ya kuhamishwa kupelekwa mahali pengine ambao walizaliana na kufikia kuku 32.
Mambo yanayomfanya mfugaji kuamua atumie njia fulani ya kufuga anasema ni pamoja na uwezo wa kugharamia shughuli ya ufugaji wa kuku na ukubwa wa eneo la kufugia.
Anasema baadaye idadi ya kuku iliongezeka na kufiki 2000 ambao hutaga mayai 600 hadi 800 kwa siku ambapo baada ya kuuza hupata sh 240,000 kwa siku moja.
Mbali ya hayo Nawanda anabainisha kuwa yai moja huuzwa kwa sh 300 ambapo kwa hesabu hiyo hupatia kiasi cha sh 7, 200,000 kwa mwezi.
Nawanda anasema bei ya kuku wa kienyeji kwa mfugaji anayeanza haizidi sh 5,000 kwa maeneo ya mijini lakini kwa Singida vijijini ni sh 2000 lakini pia mahitaji yaliyopo sokoni hivi sasa ni makubwa kutokana na jamii kutambua umuhimu wa kuku wa kienyeji kiafya.
Nawanda anasema ufugaji wa kuku wa kienyeji haumpasui mfugaji kichwa kwani huachwa wenyewe kujitafutia chakula na maji.
“Mara chache sana mfugaji huwapatia kuku chakula cha ziada ingawa kwa ufugaji huu lazima kuwe na eneo kubwa la kutosha kuku kuzunguka na kutafuta chakula,”anasema Nawanda.
Anasema kuku wa kienyeji ni rahisi ya kufugwa, gharama yake pia ni ndogo, wanapata mazoezi ya kutosha na wanapata chakula mchanganyiko kinachofaa kiafya lakini pia kikubwa ni kuingiza kipato.
Nawanda anasisitiza ufugaji wa kuku wa kienyeji katika wilaya yake na kutamba kwamba ufugaji huo umeipatia maendeleo makubwa ikiwemo bima ya afya.
Vilevile anasema ufugaji huo wa kuku wa kienyeji umesaidia kuondoa tatizo la uhaba wa dawa katika zahanati na hospitali wilayani Iramba.
Mbali ya hayo Nawanda anasema hata katika sula la makazi bora wananchi wake wamefanikiwa sana kwa sababu ya ufugaji wa kuku wa kienyeji.
“Leo hii ninajivunia kuwa mkuu wa Wilaya ya Iramba ambaye nimefanikiwa kimaendeleo kupitia ufugaji wa kuku lakini pia kuna mkakati wa kuanzisha kituo cha mafunzo kwa ajili ya ufugaji wa kuku na pia napenda kusisitiza kwamba asiyetaka kufuga kuku ahame wilayani kwangu,” anahitimisha Nawanda.
Mtaalamu wa kufuga kuku wa kienyeji Eva Kway mkazi wa Pugu nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam anasema ukiamua kufuga katika banda utatakiwa kujenga banda lenye sifa zitakazokidhi mahitaji ya msingi ya kuku.
Banda bora la kuku linatakiwa kuwa na jengo imara, pasiwe na sehemu zilizo wazi kwenye msingi na kati ya ukuta na paa, banda lijengwe na vifaa vinavyopatikana katika mazingira yako ili liwe na gharama utakayoweza kumudu.
Vilevile unaweza kutumia matofali ya udongo, miti au fito.
Anasema jengo imara litazuia wezi, panya, vicheche, paka na nyoka kuingia ndani ya banda na kuwadhuru au kuiba kuku.
Anasema banda la kufugia kuku ni lazima liwe rahisi kusafisha hususani kuta na sakafu zisiribwe ili kusiwe na nyufa.
Mbali ya hayo Kway anasisitiza uimara wa jengo ni muhimu ili kudhibiti wadudu wa kujificha katika nyufa kama papasi na viroboto.
“Sakafu ya banda lazima iwekewe matandazo kama pumba za mpunga, maranda ya mbao, mabaki ya mazao au nyasi kavu kutegemeana na kinachopatikana kwa urahisi katika mazingira yako,” anasema Kway
Anasema matandazo haya husaidia kunyonya unyevu unaotokana na kinyesi cha kuku au maji yanayomwagika katika banda.
Kway anasema banda hubakia kavu bila kuwa na harufu mbaya na wadudu kama inzi hata vimelea vya magonjwa hudhibitiwa.
Anasema eneo la nje kuzunguka banda ni lazima liwe na usafi wa kudumu kuzuia wadudu kama siafu au mchwa wasipate upenyo wa kuingia ndani ya banda.
Hasara
Kway anasema kuku huwa hatarini kuibiwa au kudhurika na wanyama wakali na hali mbaya ya hewa.
Ufugaji wa kuku wa kienyeji mbali ya kuwa na faida kubwa lakini ni hafifu, hufikia uzito wa kilo 1.2 baada ya mwaka.
Kuku hao pia huharibu mazingira kama kula mimea ya bustani, mazao kama nafaka na pia ni rahisi kuambukizwa magonjwa.

Ni rahisi kutunza kuku wa kienyeji

Unaweza kutunza kuku wa kienyeji na ukawa na kipato cha uhakika, pamoja na lishe nzuri kwa ajili ya familia.


Ulishaji: Kuku wa kienyeji wanaweza kulishwa kwa kumia mahindi, mchele, na mabaki ya ugali. Vyakula hivi ni lazima vikaushwe vizuri na kusagwa vizuri. Ulishaji ni lazima ufanyike katika sehemu safi au kwa kutumia vyombo vilivyotengenezwa maalumu kwa ajilii ya kulishia kuku.


Banda: Kuku wawe wa kienyeji au wa kisasa, wanahitaji kuwa na banda zuri kwa ajili ya malazi na kuwalinda. Wanahitaji chumba chenye nafasi ya kutosha na kinachopitisha hewa ya kutosha. Ni lazima kuwawekea fito kwa kuwa ndege hupenda kupumzika juu ya fito. Ni lazima banda la kuku lifungwe vizuri nyakati za usiku ili kuzuia wanyama wanaoweza kuwadhuru kuku. Ni lazima liwe safi wakati wote ili kuzuia magonjwa kama vile mdondo na mengineyo. Usitumie pumba za mbao au nguo kuukuu kwenye viota vya kutagia kwani huchochea kuwepo utitiri na funza wa kuku. Inashauriwa kutumia mchanga laini.


Maji ya kunywa: Kuku wapatiwe maji safi. Ni lazima kuangalia mara kwa mara na kuyabadilisha maji. Kamwe usiwape kuku maji machafu.


Chanjo: Chanjo kwa mifugo ni lazima ili kuzuia mashambulizi ya magonjwa. Magonjwa yaliyozoeleka ni kama vile Mdondo, Kideri, Ndui ya kuku, na homa ya matumbo (typhoid). Chanjo kwa kawaida hutolewa mara moja kwa kila baada ya miezi miwili.


Uwekaji wa kumbukumbu: Kumbukumbu zijumuishe aina ya ulishaji, namba ya uzalishaji, muda wa mwisho wa matumizi, kiasi cha malisho kwa kila siku, idadi ya vifo, na idadi ya mayai yaliyozalishwa.


Mwanzoni unahitaji nini?


Wafugaji walio wengi wanauliza wanahitaji nini katika hatua za awali ili kuweza kuanzisha mradi wa ufugaji wa kuku. Hii itategemea aina ya kuku uliochagua kufuga.


Ni busara kuwa na vifaa muhimu vinavyohitajika na viwe katika hali ya usafi kabla ya kuweka kuku bandani mwako. Kama unaanza na vifaranga, vifuatavyo ni vifaa muhimu vinavyohitajika kwa ajili ya vifaranga 200.


• Tenga na utengeneze banda zuri lenye joto na hewa ya kutosha wakati wote.
• Vyombo vinne (4) vya kunyweshea maji, hii ni katika wiki 2 za mwanzo na uongeze vyombo taratibu kulingana na kuku wanavyokua.
• Vyombo vinne (4) vya kulishia chakula, na viongezeke kulingana na kuku wanavyokua.
• Matandazo makavu na safi, inaweza kuwa maranda au mabua ya ngano.
• Pakiti moja au mbili za dawa ya Coccid (hii inapatikana katika maduka yote ya kilimo). Hata hivyo, utaratibu wa chanjo ni lazima ukamilishwe.
• Chakula kwa ajili ya vifaranga ambacho kimezalishwa na watengenezaji wanaoaminika.

Alhamisi, 22 Mei 2014

KILIMO BORA CHA ZAO LA NYANYA.

SOMO LA KWANZA KILIMO BORA CHA ZAO LA NYANYA
I. MUHTASARI.
Nyanya ni mojawapo ya mazao makuu ya kilimo cha mbogamboga ulimwenguni na hushika nafasi ya 2 baada ya viazi mbatata. Hapa nchini Tanzania nyanya hulimwa kwa wingi karibu mikoa yote hususani mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Morogoro, Iringa, Mwanza, Dodoma, Pwani na mbeya.

LISHE.
Matunda ya nyanya zilizoiva hutupatia:- § Vitamini A,B na C § Madini aina ya chokaa. § Maji - 94% § Utomwili(Protini )– 1% § Mafuta – 0.1% § Wanga – 4.3% § Nyuzi nyuzi (Fibres) – 0.6%

MATUMIZI.
Nyanya hutumika kama:- § Kiungo cha kupukia. § Huliwa ikiwa mbichi kama kachumbari. § ………………………………………………………………… …... § ………………………………………………………………… …… § ………………………………………………………………… …..
CHANZO CHA ZAO LA NYANYA.
Mmea wa nyanya uligundulika huko Amerika ya kati na kusini, baadaye ukaenea katika mabara mengine, ulizalishwa huko Mexico na kuletwa hadi Ulaya na baadaye ukasambaahadi kwenye nchi za tropiki.

II. MAZINGIRA.
Nyanya hustawi katika udongo wa aina nyingi ili mradi uwe na wepesi na usiotuamisha maji. (PH 5 – 7) Hali ya unyevu na joto jingi la usiku huleta majani mengi na matunda machache. Joto ni kati ya 18oC -30oC.Vilevile joto jingi, mwanga kidogo pamoja na hali ya unyevunyevu husababisha:- § Magonjwa mengi kuenea. § Mmea kuwa na majani mengi. § Matunda madogo ambayo huchelewa kukomaa. Zao ili hupendelea mvua za wastani pamoja na kipindi kirefu cha jua.Hali ya mvua nyingi pamoja na baridi kali husababisha kuenea kwa magonjwa na wadudu waharibifu.Hii ndio sababu nyanya zinazozalishwa kwa kilimo cha umwagiliaji huwa na mavuno mengi yenye ubora kuliko wakati wa mvua.

III. AINA ZA NYANYA.
 Zipo aina za nyanya zinazolimwa hapa nchini zinazofahamika na wakulima wengi ambazo hutoa mavuno mengi na bora, zinazostahimili magonjwa, zinazokomaa mapema na zenye ladha nzuri, umbo la kuvutia. Aina hizo zimegawanyika katika makundi makuu mawili kutegemea ukuaji wake. Aina fupi: Roma, Dwarf germ, ……………………………………………….. Aina ndefu:-Moneymaker, ………………………………………………………..

IV. KUSIA MBEGU. 
Mbegu za nyanya huoteshwa kwanza kwenye kitalu na baadaye huhamishiwa shambani.Matayarisho ya kitalu hufanyika wiki 1 au 2 kabla ya kusia mbegu. Tengeneza tuta lenye upana wa mita 1 na urefu wa kuanzia mita 5 hadi urefu unaoweza kuhudumia kwa urahisi. Vunja mabonge makubwa kwa kutumia jembena kulainisha udongo vizuri.Changanya mbolea za asili zilizooza vizuri kama vile Samadi au mboji kiasi cha debe 1- 2 katika eneo la mita mraba 1. Sawazisha kwa kutumia reki au kifaa kingine. Mwagilia kitalu siku moja kabla ya kusia, kisha sia mbegu katika mistari yenye nafasi ya sentimita 10 – 15 kutoka mstari hadi mstari. Kiasi kinachotosha eneo la mita mraba 1 ni gramu 3 – 5 (sawa na nusu kijiko cha chai hadi kimoja) Kiasi hiki cha mbegu huweza kutoa miche inayoweza kutosha kupandikiza katika eneo la mita mraba 100. Kiasi cha mbegu kinachohitajika kwa hekta 1 ni gramu 300. Weka matandazo kama vile nyasi kavu na kasha mwagilia maji asubuhi na jioni mpaka mbegu zitakapoota.Mbegu huota baada ya siku 5 – 10. Ondoa matandazo baada ya mbegu kuota na endelea kumwagilia maji hadi miche itakapofikia kupandikizwa.Jenga kichanja ili kzuia jua kali na matone ya mvua yasiweze kuharibu miche michanga.

V. KUTAYARISHA SHAMBA.
 Matayarisho ya shamba kwa ajili ya kupandikiza miche ya nyanya yaanze mwezi 1 kabla.Katua ardhi katika kina cha kutosha hadi kufikia sentimita 30. Lainisha udongo kwa kuvunja mabonge makubwa kwa kutumia jembe. Weka mbolea ya asili wiki 2 kabla ya kupandikiza. Tani 20 kwa hekta 1 (sawa na ndoo 1 – 2) kwa mita ya mraba.Hii ni muhimu sana kwani zao la nyanya huhitaji chakula kingi toka kwenye udongo.(heavy feeders).

VI. KUPANDIKIZA.
 Upandikizaji wa miche shambani hufanyika baada ya wiki 4 – 6 tangu kusia mbegu kitaluni na hutegemea hali ya hewa.Siku ya 10 – 14 za mwisho kwenye kitalu izoeshe miche hali halisi ya shambani.(hardening off). Wakati huu ipatie miche maji na ondoa kivuli. Mwagilia maji kwenye kitalu kabla ili kurahisisha ungoaji wa miche na kuepuka kukata mizizi. Pia ni muhimu kumwagilia shamba siku moja kabla ya kupandikiza. Iwapo mbolea za asili hazikutumika wakati wa kutayarisha shamba unashauriwa kuweka mbolea ya mchanganyiko (NPK 5.10.5) kiasi cha gramu 5 kwa shimo wakati wa kupandikiza.Baada ya kungoa miche kitaluni usichelewe kuipandikiza, pandikiza muda wa asubuhi sana au jioni ili kuepuka jua kali linaloweza kunyausha miche. Wakati wa kupandikiza hakikisha mizizi haipigwi na jua kwa kuiweka kwenye ndoo au chombo chochote chenye udongo wa unyevunyevu. Pandikiza miche katika kina cha sentimita 2 – 3 zaidi ya ilivyokuwa kwenye kitalu, hii husaidia:- § Kupata mizizi mingi mipya. § Kunyonya viini lishe. § Miche kukua kwa nguvu zaidi. NAFASI: Nafasi zinazotakiwa kutumika kwenye miche shambani hutegemea na:- § Aina ya nyanya. § Kama mimea ya nyanya itawekewa miti. § Kama itaondolewa machipukizi. § Rutuba iliyoko kwenye udongo. Aina fupi ya nyanya: hupandikizwa katika nafasi ya sentimita 90 x 50 kutoka mstari hadi mstari na sentimita 50 toka mche hadi mche. Nafasi kati ya tuta ni sentimita 60. Aina hii haihitaji kuegeshwa miti. Aina ndefu inayohitaji kuegeshwa kwenye miti hupandikizwa katika nafasi zifuatazo:-sentimita 75 mstari hadi mstari na sentimita 50 – 60 toka mche hadi mche.

VII. KUTUNZA SHAMBA
 § Kuweka matandazo. Baada ya kuhamisha miche shambani weka matandazo ili kuhifadhi unyevu na kuzuia magugu. Pia husaidia mmomonyoko wa udongo na kutunza rutuba, pia hupunguza udongo kurukia kwenye matunda na kuyaacha katika hali ya usafi. Nyanya zenye matandazo huzaa matunda yaliyo bora zaidi. § Kusimika miti ya kuegesha mimea ya nyanya. Wiki 2 baada ya kupandikiza simika miti ya kuegeshea nyanya, miti ni muhimu iwe imara na isiyooza wala kuanza kuota.Simika miti kiasi cha sentimita 8 – 10 toka kwenye sina la mmea. Mti usimikwe upande wa nje wa mstari ili kuzuia kuumiza mimea wakati wa kuhudumia.Kisha ushindilie mti sentimita 20 – 50 kwenda chini ya ardhi.Mti uwe na urefu wa mita 1.5 – 2 na unene wa sentimita 2 – 3. § Kufunga nyanya kwenye miti. Aina ndefu ya nyanya ni lazima ifungiwe kwenye mti ili:- § Kuzuia mmea usitambae chini. § Kurahisisha unyunyuziaji wa dawa. § Umwagiliaji wa maji. § Uchumaji matunda. Muhimu: Wakati wa kufunga kamba, isiwe imekazwa sana na wala isiwe imelegea kupita kiasi. Kamba ifungwe umbo la nane kati yam mea na mti.Kamba ya katani au ya mgomba huweza kutumika. Funga kamba chini ya jani kila baada ya sentimita 20 – 25. § Kuondoa machipukizi: Kwa aina ndefu ya nyanya ni muhimu kuondoa machipukizi kila mara baada ya wiki 1. Muda mzuri ni asubuhi.Ondoa machipukizi yote na acha shina 2 tu. Usitumie kisu au mkasi bali vunja kwa mkono ili kuepuka kueneza magonjwa ya virusi na bacteria. Sababu za kuondoa machipukizi: - Huchukua chakula cha mmea. - Mmea hutoa matunda mengi madogo ambayo hayafai kwenye soko. § Kuondoa Majani: Ondoa majani yote yanayoonyesha dalili zote za magonjwa au kushambuliwa na wadudu, yale yote yaliyozeeka ili kupunguza hali ya unyevu na kuruhusu hewa ya kutosha kwa mimea. Majani yote yaliyoondolewa yachomwe moto ili kuliweka shamba katika hali ya usafi. § Kukata kilele: Kwa kawaida aina ndefu ya nyanya huzaa ngazi 6 – 8 za matunda lakini mmea una uwezo wa kubeba ngazi 5 – 6. Hivyo ni muhimu kukata sehemu ya juu yam mea (kilele) ili kusimamisha ukuaji wake. Hii husaidia chakula kingi kwenda kwenye ngazi chache na hivyo kupata matunda makubwa. Kata kilele wakati mimea ifikiapo ngazi ya 6 na usikate karibu sana na ngazi na kata mkato wa mlalo ili kuruhusu maji kutiririka. Hata hivyo kama udongo una rutuba nyingi sana unaweza kuachia hata ngazi 8. § Palizi: Palilia mara kwa mara kwa kupandishia udongo kwenye shina kwa uangalifu ili kuepuka kukata mizizi. Palizi husaidia maji na hewa kupenya kwa urahisi kwenye udongo. Hata hivyo kama mimea imewekewa matandazo ya kutosha na haina miti ya kuegeshea ni vyema palizi ikaachwa ili kuepuka kuumiza matunda. § Kumwagilia maji: Kwa kawaida nyanya hutoa mazao mengi wakati wa kiangazi kuliko wakati wa mvua za masika.Mwagilia maji ya kutosha mara 2 kwa siku hasa wakati matunda ya kwanza yanapoanza kutunga. Kumwagilia maji mengi kupita kiasi au kidogo sana husababisha matunda yawe na hitilafu ya kupasuka. § Kuweka mbolea ya kukuziatop dressing). Mbolea zenye nitrogeni ndio hutumika kwa kukuzia,mfano S/A,UREA au CAN na hutumika wiki 2 – 4 tangu kupandikiza miche kwani inakuwa tayari na mizizi mipya itakayonyonya mbolea hiyo. Mbolea hii ya kukuzia huwekwa mara 2. Mara ya kwanza weak gramu 5 kwa kila mmea za SA au CAN. Rudia tena wakati inaanza kutoa matunda. Muhimu: Kiwango cha nitrogeni kinatakiwa kidhibitiwa na kurekebishwa ili kitumike kiasi kile tu kinachohitajika vinginevyo mimea itakuwa na majani mengi sana yenye afya bila matunda na itachelewa kukomaa na kuiva kwa matunda.

VIII. MAGONJWA: 
Nyanya ni zao ambalo hushambuliwa sana na magonjwa mbalimbali. § Magonjwa ya ukungu (Early blight): Ambukizo:- Fungusi aitwae Altenaria solani. Dalili: Majani: Kingo za majani huwa na madoa ya rangi nyeusi iliyochanganyika na kahawia, pembe zake huwa za njano. Shina: Huwa na madoa kama ya kwenye majani lakini makubwa na kusambaa zaidi.Baadaye madoa hupanuka na kuwa mabaka makubwa ya rangi nyeusi, makavu na yaliyodidimia,shina huwa jembamba, usawa wa ardhi na hudumaa na huvunjika kwa urahisi. Matunda: Huwa na madoa meusi ya mviringo yenye umbo la yai.Madoa huonekana zaidi kwenye kikonyo cha tunda na kwenye sehemu iliyopasuka. Kadri tunda linavyozidi kuiva madoa haya huongezeka zaidi. § Bakajani (late blight) Ambukizo: Phytophthora Infestans. Dalili za ugonjwa huu huanza kuonekana kwenye jani la chini. Majani na shina huwa na mabaka makubwa yenye rangi nyeusi au kahawia nzito. Katika hali ya unyevunyevu, majani huoza na hatimaye uyoga mweupe huonekana chini ya jani. Baadaye majani huakuaka na kuwa yameunguzwa na moto. Matunda yaliyopatwa na ugonjwa huu huwa madoa ya rangi ya kijani iliyochanganyikana na kahawia. Baadaye huwa makubwa na kuoza, ukipasua tunda lilooza utaona weusi. Nyanya zenye ugonjwa huu zikihifadhiwa kwenye sehemu zenye unyevunyevu, hutoa uyoga mweupe. Jinsi unavyoambukizwa na kuenea:- Ukungu wa ugonjwa huu hutokea kwenye majani ama shina huambukizwakutoka mmea hadi mmea kwa njia ya upepo, mvua na umwagiliaji wa majai ya mashambani. Kuzuia Ugonjwa wa Bakajani:- - Kubadilisha mazao, usipande nyanya katika eneo moja mfululizo. - Kuweka matandazo shambani - Kupunguzia matawi na kuondoa majani yaliyoshambuliwa. - Kung’oa masalia yote shambani mara baada ya kuvuna na kuchoma moto. - Sia mbegu katika kitalu kilichotayarishwa vizuri. - Tumia mbegu bora ambazo hazijashambuliwa na ugonjwa. - Otesha aina ya nyanya zinazovumilia mashambulizi ya ugonjwa huu. - Tumia dawa za ukungu kama vile Dithane M-45, Ridomil, Tposin M70, Copper Oxichloride (Cipro), Cupric Hydroxide, (Champion) § Mnyauko Bakteria:- (Bacteria Wilt) Ambukizo:- Pseudomonas Solanacerium Mmea ulioshambuliwa hunyauka ghafla bila kuwa njano hasa wakati wa jua kali na njano. Baadaye mmea hudumaa majani na vikonyo vyake hukunjamana, shina likikatwa karibu na usawa wa ardhi rangi ya kahawia nzito huonekana kwenye sehemu ya kusafirishia maji. Sehemu iliyokatwa ikiwekwa kwenye maji uji mzito kama maziwa huchuruzika. Jinsi ugonjwa unavyoambukizwa na kuenea:- Ugonjwa huu huwa katika udongo na kujitokeza zaidi wakati wa joto na pale ardhi ikiwa na unyevenyevu. Huweza kuishi ardhini muda mrefu katika masalia ya mimea ya nyanya na kushambulia mimea mingine. Ugonjwa ukishakuwepo ardhini huenea haraka kwa njia ya umwagiliaji maji na maji ya mvua kufuata mteremko wa ardhi. Pia huenezwa toka mmea hadi mmea kwanjia ya mizizi kugusana. Kuzuia ugonjwa:- - Otesha mbegu kwenye kitalu ambacho hakina ugonjwa huu. - Epuka kupanda nyanya kwenye sehemu ambayo ina ugonjwa huu. - Badilisha mazao shambani - Otesha nyanya zinazostahimili ugonjwa huu. - Ng’oa na choma moto mimea yote iliyoathirika na usipande tena nyanya au jamii yake kwa kipindi cha miaka 4- 5. § Mnyauko Fuzari ( Fuzarium Wilt) Ni ugonjwa wa ukungu. Husababisha majani kuwa rangi ya njano na mimea kunyauka hasa wakati wa jua kali, majani yaliyoshambuliwa huvunjika kwa urahisi. Kama shina likinyofolewa karibu na usawa wa ardhi rangi ya kahawia huonekana. Mmea: Hunyauka ----- huwa njano --- hufa. Kuzuia ugonjwa: - Kung’oa mimea iliyoshambuliwa na kuichoma moto. - Otesha aina ya nyanya zenye ukinzani kama vila Roma, VFM, n.k. - Tumia dawa kama vile Topsin M70, dawa inyunyiziwe kwenye udongo. § Batobato (Tomato Mosaic Virus) Husababishwa na virusi. Hushambulia majani machanga na yaliyozeeka. Majani yaliyoshambuliwa hukunjamana na kudondoka. Hali kadhalika majani yaliyozeeka huvunjika kwa urahisi na huwa na rangi nyeusi, kijivu au kikahawia china ya jani. Mwisho majani kuhakauka na kufa. Zuia ugonjwa kwa yafuatayo:- - Epuka kuotesha nyanya kwenye eneo lililoathirika - Ng’oana choma moto mimea yote iliyoshambuliwa. - Otesha mbegu zilizodhibitishwa kitaalamu - Epuka kuhudumia mimea mingine baada ya kuhudumia ile iliyoathirika. osha mikono kabla ya kuhudumia mingine. - Safisha vifaa vyote kama vile visu, mikasi kwa maji na sabuni baada ya kuvitumia. - Usivute sigara ndani ya shamba la nyanya. - Otesha aina ya nyanya zinazostahimili magonjwa ya batobato. § Ugonjwa wa madoa jani (Septoria leaf spot) Husababishwa na ukungu na kushambulia majani na kuwa na madoa meusi na kingo zake huwa na rangi ya kijivu iliyoambatana na madoa meusi. Kuzuia:- - Nyunyiza dawa za ukungu kama vile Dithane M45, Blitox na Coper fungicides. § Scleretonia Rot: Ambukizo: Ni mdudu aina ya fungusi aitwaye sleratinia scerotirum. Dalili za ugonjwa:- Muozo mwepesi katika shina ikifuatiwa na unyaukaji wa ncha za mmea na matawi. Wakati wa unyevunyevu, viini vyeupe vya fungusi hutokea katika sehemu zilizoshambuliwa na ugonjwa. Viini vikubwa vya ugonjwa vigumu na vyenye rangi nyeusi huwepo ndani ya mmea ulioshambuliwa na kisha mmea mzima hunyauka na kufa au hukauka. Jinsi unavyoambukiza na kuenea: Fungusi wa ugonjwa wana uwezo wa kuishi ardhini kwa muda mrefu. Nyakati za baridi na unyevunyevu wale waliokuwa usawa wa ardhi huzaana kwa wingi na kisha kupeperushwa na upepo. Ugonjwa unaambukizwa pale ambapo maua makavu na majani yenye ugonjwa yakigusana na sehemu za mimea isiyo naugonjwa. Ugonjwa huu hutokea zaidi wakati wa mvua, baridi na nyakati za ukungu na umwagiliaji ndipo ugonjwa huenea zaidi. Mimea mingi ilimwayo na majani hushambuliwa sana na ugonjwa huu. Kuzuia:- - Tumia dawa za aina ya fungicide. - Epuka kupanda mimea katika eneo lililoshambuliwa sana na ugonjwa hasa wakati wa baridi.

HITILAFU ZA MATUNDA
 Kupasuka matunda: Kuna aina mbili za mipasuko; mpasuko wa mviringo na mpasuko wa nyota. Mpasuko wa mviringo: Hutokea wakati mmea haukupata maji ya kutosha hasa wakati wa jua kali. Wakati huu maji yaliyoko kwenye tunda hayawezi kulingana na maji yanayopotea angani kama mvuke. Mpasuko wa umbo la nyota: Hutokea hasa tunda linapokuwa na maji mengi na wakati huo unyevu angani ni mwingi sana. Hivyo tunda hushindwa kupoteza maji kwa njia ya mvuke na hupasuka kabla ya kukomaa. Hutokea zaidi kwenye nyanya aina ya Marglobe. Mpasuko wa mviringo na umbo la nyota huzuiwa kwa kumwagilia maji ya kutosha. § Kuoza kitako: Vidonda vyeusi vilivyodidimia huonekana kwenye kitako cha tunda. Sehemu hii baadaye hunyauka na ngozi huwa nyeusi. Hali hii hutokea zaidi wakati wa jua kali na katika sehemu zenye udongo wenye chumvichumvi na tindikali nyingi. Zuia hali hii kwa kuhakikisha udongo una unyevunyevu wa kutosha wakati wote. Pia epuka kuweka mbolea nyingi za chumvichumvi. § Mabaka ya matunda: Matunda yaliyopigwa na jua kali huwana mabaka hasa sehemu za ubavuni. Hali hii inaweza kuzuiwa kwa kuepuka kupunguza matawi mengi kwa wakati mmoja. § Matunda ya kijani kibichi: Mabega ya tunda huwa na kijani kibichi. Hitilafu hii hutokana na chanikiwiti kuwa nyingi na hutokea hasa wakati wa jua kali. Ili kuepuka hali hii unashauriwa kutoweka mbolea nyingi ya chumvichumvi na punguza mwanga wa jua kufunika matunda na majani makavu.

WADUDU WAHARIBIFU 
 Funza wa vitumba (AmericanBollworm) Ni funza watokanao na aina Fulani ya nondo. Wana rangi ya kijani hutokea baada ya mayai ya nondo kuanguliwa, kisha hutoboa matunda na kuishi humo. Jinsi wanavyokula na kukua husababisha matunda kuoza. Kuzuia:- Nyunyiza dawa za Carbarly, Dimethiote , Sumucidin na Dichlorvos. § Utitiri (Red spider mites) Ni wadudu wadogo sana na wenye rangi ya machungwa, nyekundu au kahawia. Vijidudu hivi hushambulia kwa kufyonza utomvu chini ya majani. Majani yaliyoshambuliwa huwa na rangi ya njano, hukunjamana, hukauka na hatimaye mmea hufa. Kuzuia:- Tumia dawa aina ya Morestan, Kelthane, Dimethoate, Diazinon, Ekalux, Poltrin na Profenofos. § Vidukari/wadudu mafuta (Aphids) Ni wadudu wadogo wenye rangi ya kijani, nyeusi au kahawia. Baadhi wana mabawa wengine hawana. Hufyonza utomvu wa majani na kusababisha mmea ulioshambuliwa kudhoofika, kudumaa, majani kunyauka na hatimaye kukauka. Kuzuia:- Tumia Dimecron, Actellic 50 Ec, Selecron, Sumicidin, Karate, Dichlorvos na Dimethoate. § Minyoo fundo: Wadudu wadogo weupe ambao hawaonekani kwa macho na huishi kwenye udongo. Hushambulia mizizi na kusababisha mimea kudhoofika na kushindwa kutoa matunda. Pia husababisha matunda kuiva kabla ya kukomaa. Uking’oa mmea ulioshambuliwa utaona mizizi ina vinundunundu. Kuzuia:- Tumia mzunguko wa mazao kwenye enneo moja. Baada ya kuvuna nyanya zao litakalofuata lisiwe la jamii ya nyanya, mfano Hoho, bilinganya. Kama madhara ni makubwa sana tumia dawa ya Furadan, na dawa za kufukiza ardhini kama Curaterr, Dazomet. Kumbuka:- Kumwagilia kwa kutumia mifereji kunaweza kusambaza minyoo shambani. tukutane tana wiki ijayo kwa somo la pili kwa maoni na ushauri usisite kuniandikia ua kutoa coment

UMWAGILIAJI MAJI SHAMBANI KWA MATONE

Umwagiliaji maji mashambani kwa teknolojia ya matone (drip irrigation) ni nzuri hasa kwa kilimo cha mboga mboga kwani kiasi cha maji kidogo hutumika kuzalisha mazao kwa kuupa uhakika mmea wa kupata maji wakati unapoyahitaji. Teknolojia hii husaidia kuzalisha mazao kwa faida. Wataalamu wa kilimo wa umwagiliaji wanaweza kukusaidia kukupa maelezo ya kina kuhusu teknolojia hii.Ulizia Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika- Barabara ya Mandela/Kilimo- Temeke Veterinary, Halmashauri za wilaya, na Ofisi za Umwagiliaji za Kanda.