DONDOO ZA UFUGAJI BORA KUKU WA ASILI
Muhtasari wa ufugaji kuku wa asili ili kuzuia vifo na
kuboresha uzalishaji.
Ufugaji wa kuku wa asili ni nyenzo muhimu katika kupambana
na wimbi la umasikini kwa kuongeza kipato cha kaya. Hata hivyo, pamoja na soko
la uhakika, bado ufugaji kuku haujaweza kutumika ipasavyo kupambana na umaskini
unaowakabili watanzania wengi. Ni mazoea kwa jamii nyingi hapa Tanzania kufuga
kuku wa asili kama sehemu ya mila na desturi zao. Kuku wa asili amekuwa
akifugwa bila ya kupatiwa huduma muhimu kama makaazi bora, chakula cha ziada,
tiba, kinga za magonjwa mbali mbali . muhtasari huu unatoa muongozo wa ufugaji
wa kuku wa asili ili uweze kuzalisha na
hatimae kukuza kuku kwa wingi.
Dondoo ya 1. Usafi wa
vyombo na mazingira ya kuku
·
Uchafu ni mama wa magonjwa, hivyo zingatia haya;
·
Vyombo vya chakula na maji visafishwe mara kwa
mara kwa maji na sabuni.
·
Pumba au chakula kilicholowana na kuchanganyika
na kinyesi cha kuku vitolowe na kuzikwa.
·
Choma moto au zika kwenye shimo refu kuku waliokufa
kwa ugonjwa.
·
Usifuge kuku na ndege wa jamii nyingine kwa
mfano bata katika banda moja.
·
Ondoa mbolea mara kwa mara kutoka katika banda
la kuku.
·
Tumia dawa za kuulia vimelea kusafishia banda na
upake chokaa angalau mara moja kwa mwaka.
·
Ziba matundu yote yanayoweza kuruhusu panya na
wanyama wakali kama vicheche kuingia katika banda la kuku.
Dondoo ya 2. Magonjwa
na kinga kwa kuku wote.
Ndui ya kuku.
Huathiri sana vifaranga wanaokua na kujitokeza kwa wingi
wakati wa mvua ndefu. Husababisha vivimbe katika uso/ kishungi na hata sehemu
nyengine zisizo na mnyoa.
Mdondo/kideri
Mdondo, au kwa majina mengine lufuo, au kideri ni ugonjwa
hatari kuliko kati ya magonjwa ya kuku wa asili. Ni ugojwa wa virusi ambao
huathiri kuku wa rika zote, huweza kuangamiza kuku wote kijijni.
Ukosefu wa vitamin A
Ugonjwa huu husababisha macho kuvimba na kutoa uchafu mziito
kama sabuni iliyolowana. Kuku wenye dalili hizi hawaponi na hata kufa. Ugonjwa
hujitokeza baada ya kipindi kirefu cha kiangazi kwa ajili ya ukosefu wa majani
mbichi.
Koksidiosisi
Huathiri kuku wa umri wowote lakini huuwa zaidi vifaranga na
kuku wanaokuwa. Kuku hudhoofika manyoya huvurugika na kuku huwa kama wamevaa
koti. Kuku huarisha damu au kinyesi cha kahawia na huzubaa na kuonekana kama
wamevaa koti.
Viroboto, chawa na
utitiri
Hawa ni wadudu wa n je wanaoshambulia ngozi. Huweza
kusababisha ugonjwa kutokana na kunyonya damu. Viroboto hushambulia kichwa na
kunata huku wakinyonya damu. Viroboto huuwa vifaranga. Chawa na utitiri hughasi
kuku hadi wakashinwa kutaga na kuatamia.
Minyoo.
Minyoo huweza kudhofisha kuku na kuwafanya waweze kuugua
maradhi mengine kirahisi. Muune mtaalaam ukihisis kuku wako wana minyoo.
Dondoo ya 3. Chakula
cha ziada:
·
Wapatie vifaranga nyongeza ya protini kwa
kuwachanganyia vumbi la dagaa au vichwa l vya dagaa vilivyotwangwa kwenye pumba
za mahindi.
·
Changanya kikombe kimoja cha vumbi la dagaa na
vikombe vitano vya pumba za mahindi (tumia kikombe kidogo cha chai) .
·
Mchwa na wadudu wengine wanaweza kutumika kam
nyongeza ya protini.
·
Vuna mchwa kwenye vichuguu au tengeneza mchwa
katika njia za mchwa.
·
Kutengeneza mchwa: changanya kinyesi cha ng’ombe
na majani makavu, mabua ya mahindi au maranda ya mbao katika chungu au ndoo ya
zamani.
·
Mwagia maji hadi kila kilichomo kirowane kisha
weka katika chombo kama ndoo au chunngu. Weka chombo chako katika njia ya mchwa
ukikigeuza juu chini na subiri hadi kesho yake asubuh, kisha beba vyote
vilivyomo na uwamwagie kuku mahali walipo.
Dondoo ya 4.
Utotoleshaji wa vifaranga;
Chagua jogoo bora na
tetea bora kuzalisha kuku .
·
Sifa za jogoo bora ;
1.
Awe na umbo kubwa, awe ukiko mzuri na
usioangukia upande mmoja.
2.
Apende kuwa na himaya yake. Ukimpata jogoo
mwenye sifa hizi muweke yeye na matetea kumi. Hivyo ukiwa na matetea ishirini
jogoo wawili wanatosha.
·
Sifa za tetea bora;
Tetea bora ni Yule mwenye umbo kubwa,
mwenye uwezo wa kutaga mayai ya kutosha, kuatamia na hatimae kutotoa vifaranga
na
·
Uhifadhi wa mayai;
1.
Weka mayai mahali safi na penye hewa ya kutosha.
2.
Tumia box lililokatwa na kujaza mchanga mkavu na
safi au kasha la kuhifadhia mayai.
3.
Weka sehemu butu ya yai iwe upande wa juu na ile
iliyochongoka itizame chini.
4.
Andika namba au tarehe katika siku lilipotagwa.
5.
Mayai yakishatagwa yatolewe na kuhifadhiwa na
moja liachwe kwenye kiota ili kumuita kuku kuja kutaga kesho yake.
·
Kuatamiza mayai;
-
Kuku awekewe mayai yatakayokuwa na uwezo wa
kuyaatamia na kuyatotoa yote.
-
Mayi 10 hadi 12 yanatosha kutamia.
-
Mayai ya kutamiza yasizid wilki 2 toka kutaga.
-
Yai la mwisho kutagwa liwe la kwanza kuchaguliwa
hadi yapatikane mayai 10 mpaka 12, na apewe kuku kuyaatamia.
-
Mayi ya kutamiza yasafishwe kwa kitambaa
kikavu na safi au kilichowekwa spiriti
·
Kutotolesha vifaranga wengi kwa wakati mmoja.
-
Kama unataka kuku zaidi ya mmoja watamie na
kutotoa kwa mpigo fanya yafuatayo;
-
Kuku wa kwanza akianza kuatamia muwekee mayai
yasiyo na mbegu mfano mayai ya kuku wa kisasa au kuku asiye na jogoo.
-
Rudia zoezi hilo hadi utakapofikisha kuku watano
kasha waweke kuku wote mayai yenye mbegu.
Dondoo ya 5. Matumizi
ya vifaranga ili kuzuia vifo.
Vifaranga wengi hufa kabla ya kufikisha miezi miwili
kutokana na magonjwa, baridi na kuliwa na wanyama wengine. Ili kupunguza vifo
vya vifarang wa siku 1 hadi miezi miwili zingatia yafuatayo;
Ulinzi dhidi ya mwewe na wanyama wengine.
Weka vifarang kwenye tega na kuwafunika ili wasinde mbali
wakati wa mchana. Wape maji na chakula. Hakikisha hawapigwi jua wala kunyeshewa
mvua. Wakati wa usiku walale na mama yao.
Chanjo ya mdondo
kideri/lufuo
Kama tetea alichanjwa kabla ya kuanzakutaga vifaranga
wanaoambuliwa huwa na kinga ya dondo ya kuwatosha kwa wiki 3 za kwanza za
maisha yao. Wachanje vifaranga hao dhidi ya mdondo wafikishapo umri wa siku 18.
Vifaranga ambao historia ya chanjo ya mama haijulikani,
wapewe chanjo ya mdondo siku tatu baada ya kuanguliwa, rudia wakifikisha wiki
tatu kasha uchanje kila baada ya miezi 3
Kinga dhidi ya kiksidiosisi
Kinga ya koksidiosisi kwa vifaranga, itolewe hata kama
ugonjwa haujajitokeza.
·
Wape dawa ya aprolium kwa muda wa siku tatu
mfululizo mara wafikishapo siku saba tokea waanguliwe kama kinga ya
koksidiosisi.
·
Dawa inaweza kutolewa hata kama wamevuka umri
huo. Fuata maelekezo ya mtaalam juu ya kiasi cha dawa kinachopaswa
kuchanganwa katika maji au pumba
·
Kama vifaranga wadoga wataonesha dalili za
kuzubaa kama kuvua koti wapewe dawa ya amprolium kwenye maji kwa utaratibu
ufuatao;
Dawa siku tatu mfululizo: usiwape kwa siku
mbili; gawa tena kwa siku tatu
HITIMISHO
Hakikisha banda na vyombo vya chakula cha
kuku na visafi kuepusha magonjwa.
·
Usichanganye kuku na bata katika banda moja
·
Lisha chakula cha ziada hasa kwa vifaranga.
·
Kideri, koksidiosisi, ndui na upungufu wa
vitamin A ni vyanzo vikuu vya vifo vya
kuku wako. Kumbuka kukinga kuku wako dhidi ya magojwa haya.
·
Kumbuka kuchagua mayai ya kuatamiza kama
ilivyoelekezwa ili kuepuka kupata mayai viza.
·
Vifaranga wadogo hadi wiki nane huhitaji matunzo
mazuri fuata maelezo kuzuia vifo.
·
Kumbuka ukiuza kuku wengi kwa mpigo utaongeza
mapato yako, jitahidi kuzalisha vifaranga kwa wingi ili upate kuku wengi
baadae.
·
Muone mtaalam wa mifugo ulie karibu nae kwa
ushauri zaidi.
·
Soma maelezo haya mara kwa mara na ufanye
yalioelekezwa.
·
Washirikishe wengine katika kaya yako ili nao
wajifunze na kufanya, ivyo kukuza ufugaji na kipato cha familia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni